Maadili kwa wasanii

Jumatano , 23rd Sep , 2020

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza ameeleza kuwa maadili ni moja ya sababu moja wapo inayopelekea baadhi ya wasanii kuchaguliwa katika shughuli za kitaifa.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza

Akizungumzia hilo kupitia EATV & EA Radio Digital Godfrey Mngereza amefunguka kuwa "Wapo wasanii wengi wakike ambao wanafanya vizuri kazi zao na kufuata maadili bila kumtaja mmoja mmoja na hao ndio hupelekea kuchaguliwa katika shughuli za kitaifa na wasiofuata maadili pia wanajielewa nawaomba wajirekebishe"

Aidha ameendelea kusema "Kanuni zinazotolewa na BASATA ni kanuni za Bunge za mwaka 2018 sheria no:23 za mwaka 1979 ambazo zinatoa maelekezo ya  kuzingatia kuhusu msanii anatakiwa kufanya kabla ajatoa nyimbo katika jamii na kazi ya uhakiki inafanywa msanii mwenyewe kabla haijafika nje"