Lulu Diva amshangaa Ben Pol kudai talaka kwa Mkewe

Alhamisi , 8th Apr , 2021

Bossbaby wa BongoFleva Lulu Diva amesema mapenzi hayana adabu kwa sababu sasa hivi yupo single na anatamani kuingia kwenye mahusiano ila ameshangaa Ben Pol kudai talaka ya kutaka kutoka kwenye mahusiano ya ndoa na Mkewe Anerlisa Muigai.

Kulia ni msanii Lulu Diva, kushoto ni Ben Pol na mkewe Anerlisa Muigai

Lulu Diva ametoa kauli hiyo kwenye post yake ya mtandao wa Instagram baada ya kutoka taarifa ya msanii Ben Pol ambayo inasemekana kutaka kufungua shauri la Mahakamai kudai talaka kwa mkewe Anerlisa Muigai ambaye ni Raia wa Kenya.

"Ila haya mapenzi hayana adabu mimi nipo single ndio nataka kuingia mara nasikia ndugu yangu Ben Pol anadai talaka anataka kutoka, sasa niache au niendelee kutafuta mpenzi" ameandika msanii Lulu Diva 

Ben Pol na Anerlisa walifunga ndoa mwishoni mwa mwezi May mwaka 2020 katika Kanisa Katoliki la St. Gaspar Mbezi Beach, Jijini Dar es Salaam.