"Kupiga picha ngozi kutakupangia nguo" - Vanilla

Jumatano , 23rd Sep , 2020

Mtangazaji wa kipindi cha 5Selekt ya East Africa TV ametusanua kuhusu teknolojia ya simu inayovyoweza kutumika kusaidia kuchagua rangi za nguo zinazoendana na rangi ya ngozi ili kuleta muonekano mzuri.

Mtangazaji wa kipindi cha 5Selekt ya East Africa TV Vanilla Dama

Akifunguka hilo wakati wanazungumzia mada ya inayohusu ufahamu wa rangi ya nguo unayoivaa na bahati zake Vanilla Dama amesema kuwa, 

"Siku hizi kuna teknolojia ambayo unaweza kutumia kwa kupiga picha ngozi yako na ikakuonesha ni aina gani ya ngozi uliyonayo kisha kukuchagulia rangi za nguo zinazoendana na ngozi yako sio kitu cha kushangaza ila ni chakujifunza kuwa tunaenda na wakati inabidi tubadilike ili tusichanganye mambo".

Zaidi tazama hapa chini kwenye video