Jumatatu , 20th Sep , 2021

Msanii kutoka lebo ya Kings Music Records Abdukiba ambaye anasema TP Mazembe wameharibu sherehe yao kwenye siku ya Simba Day ila ndio matokeo ya mpira.

Picha ya msanii Abdukiba

Abdukiba ameongeza kusema matokeo hayo yamewafanya kuwa wanyonge hivyo harudi  nyumbani kwa kuhofia fujo za kaka yake Alikiba ambaye ni shabiki wa Yanga.

Mwisho amesema timu yake ni nzuri japo wanahitaji kupata nafasi na muunganiko, pia ametabiri matokeo ya mchezo unaofata dhidi ya Yanga kwenye ngao ya jamii kwa kusema Simba atashinda 3 bila kwa hasira za TP Mazembe.

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video