Kinachoendelea kwa Roma nchini Marekani 

Jumanne , 13th Oct , 2020

Kwa muda mrefu sasa msanii wa HipHop Roma Mkatoliki anaishi nchini Marekani, mashabiki wengi wanajiuliza anafanya shughuli gani ili kuweza kumuingizia kipato ambacho kitaweza kumudu maisha ya Marekani pamoja na kusaidia familia yake aliyoicha Tanzania.

Msanii Roma Mkatoliki kushoto, kulia ni Promota DMK

Sasa huyu hapa ni Promota wa kimataifa DMK anayoosha maelezo kuhusu kinachomtatiza msanii huyo kufanya show nchini huko ili ajipatie fedha za kufanya mambo mengine.

"Ili msanii aweze kufanya show Marekani anatakiwa awe na 'paper work' ambazo zitamruhusu kufanya kazi Marekani pia awe na kibali cha kufanyia kazi, Roma Mkatoliki hakuja kwa ajili ya show alikuja kwa ajili ya tukio la Swahili Society USA" amesema Promota DMK 

"Roma Mkatoliki hawezi kufanya show Marekani kwa sababu visa yake iliyomruhusu ilikuwa tofauti hata kama kuna mtu anataka afanye naye show, lazima arudi kwanza Tanzania achukue kibali cha kazi  na 'Proper Visa' kisha ndiyo akafanye show Marekani" ameongeza 

Roma Mkatoliki ameenda Marekani mwishoni mwa mwaka 2019 kwa ajili ya tukio la 'Swahili Society USA' ambapo huku Tanzania ameacha watoto wawili pamoja na mkewe Mrs Roma.