Jux amkosesha Bright penzi la Vanessa

Monday , 15th May , 2017

Chipukizi anayefanya vizuri kwa sasa, Bright ameweka wazi kuwa ndoto za kuwa na mahusiano ya kimapenzi msanii Vanessa Mdee bado hazijafutika na kusema kama mrembo huyo asingekuwa na mahusiano ya kimapenzi na Jux, yeye angeshamchukua mrembo huyo.

Bright amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa radio kwamba, kuwa na Vanessa ni ndoto yake ya siku nyingi ila inashindwa kutimia kutokana na uwepo wa Jux.

“Unajua mawazo huwa hayafi ndio maana watu wanakufa na ndoto zao ndivyo ilivyo hata kwangu, mimi naamini kama itatokea siku moja napata nafasi ya kuwa naye nitafurahi lakini naona pale kuna mtu kama kang’ang’ana sana . Ila ikitokea nafasi fresha mimi namchukua, nitajiongeza amesema Bright.