Jimmy Kindoki awatangazia Simba 'War In Zanzibar' 

Ijumaa , 8th Jan , 2021

Ni mbwembwe za mwanachama na shabiki wa Klabu ya Yanga Jimmy Kindoki ambaye amewatangazia vita watani wake wa jadi Klabu ya Simba kwamba kutakuwa na vita nyingine huko kwenye kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.

Shabiki wa Yanga Jimmy Kindoki kushoto, kulia ni wachezaji wa Simba

Kupitia EATV & EA Radio Digital, Jimmy Kindoki amesema kwa kuwa Simba wamemaliza vita ya kwanza hapa Jijini Dar Es Salaam 'War In Dar' dhidi ya FC Platinum basi kutakuwa na vita nyingine ya 'War In Zanzibar' endapo watakutana kwenye kombe hilo.

"Si wamekuja kule Mapinduzi tutakutana nao, pia waje na hao paka,fisi na kuku waone, tunawataka Simba hata kesho ili tujue nani ni mbabe wa mwenzie kwa msimu huu, wao si wametangaza 'War In Dar' na sisi tunasema 'War In Zanzibar' tutawashughulikia" amesema Jimmy Kindoki 

Zaidi tazama mbwembwe za shabiki huyo kwa kubonyeza hapo chini.