Jumamosi , 2nd Jan , 2021

Ni 'headlines' za msanii wa filamu na mfanyabiashara Jacqueline Wolper ambaye kupitia post zake mbili za mwisho kwenye mtandao wa Instagram ametangaza kuwataja mastaa 10 ambao anawadai na wamegoma kumlipa pesa zake.

Msanii wa filamu Jacqueline Wolper

Kupitia post hizo Jacqueline Wolper ameandika kuwa "Haya tangazo tangazo, wote mliokopa kwangu Mwaka jana nawapa hadi saa 10 jioni kama hamjalipa nawaanika kweupe ili wengine wakiona sura zenu wafunge maduka yao, tuonane kesho kuna 'top 10' nitawapost wote na nguo zangu mnazojishauwa nazo kenge nyie

"Leo nimelipwa hizo milioni kadhaa hapo 'atleast' na mimi nikalipe, sasa bado wale magwiji wavikoba mastaa pumbavu kabis,a nina hasira nao kuliko chochote hawa sijui tuwape siku ngapi" ameongeza 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.