Harmonize na Kajala wachorana Tattoo kwenye shingo

Ijumaa , 19th Feb , 2021

Kwenye msimu huu wa makopakopa na malavidavi msanii na boss wa Konde Gang Music, Harmonize na mpenzi wake Kajala Masanja wamenogesha mahaba kwa kuchorana 'Tattoo' zenye herufi ya mwanzo ya majina yao.

Tattoo walizochora Harmonize na Kajala kwenye shingo zao

Wawili hao wamechora Tattoo hizo kwenye shingo zao ambapo Harmonize ameandika herufi ya jina la Kajala kwa maana ya 'K' na mpenzi wake Kajala  Masanja naye ameandika herufi 'H'.

Kwa sasa penzi la Harmonize na Kajala ndiyo linazungumziwa zaidi kwenye habari za kiburudani na siku ya Valentine walienda Visiwani Zanzibar kula bata, pia msanii Harmonize amemtungia wimbo wa kumsifia mpenzi wake huyo.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.