Jumatano , 18th Nov , 2020

Msanii na Boss wa lebo ya Konde Gang Music Harmonize amewaunga mkono ma-Dj's wa kitanzania kwa kutocheza miziki ya kibongo kwenye kumbi za starehe kwa kusema wasanii wanataja sana viungo vya pilau kwenye nyimbo zao.

Msanii na boss wa Konde Music Worldwide Harmonize

Akieleza hilo kupitia 'Insta Story' yake Harmonzie amesema anajivunia ma-producer wa Tanzania wana uwezo wa kufanya vizuri na wana vipaji ila kilichobakia ni kufanya maamuzi ya kubadilisha muziki wanaoufanya.

"Napenda jinsi ma-dj's wa Tanzania kutocheza sana muziki wa Bongo Club, tunataja sana viungo vya pilau kwenye ngoma zetu, tunatakiwa kubadilika tunawapa shida waache kupiga nyimbo kama mazerati, no stress, woman au mapiano sound halafu wakapige pembe la ng'ombe ukiuliza ni uzalendo, hivyo tutakuwa hatutangazi bali tunaua lugha yetu nzuri ya Kiswahili kwa sauti mbaya tunazozitumia" ameeleza Harmonize 

Aidha ameongeza kueleza kuwa "Nawaamini ma-producer wa Tanzania kwa asilimia 100, kipaji ni msanii kufanya uamuzi na kutengeneza njia za huu muziki kuwa burudani ya kweli, tunahitaji kubadilika tunaweza kukimbiza dunia"