Hanstone naye aambulia kipigo hadi kuumizwa

Alhamisi , 15th Oct , 2020

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hanstone amesema na yeye ni mmoja wa watu ambao walivamiwa na kupigwa hadi kuumizwa kwenye studio za mtayarishaji wa muziki S2Kizzy iliyopo Sinza Lion.

Msanii wa BongoFleva Hanstone

Hanstone amesema amepigwa bila hatia na kuvamiwa na watu hao ambao walijitambulisha kama polisi jamii kisha kuwapiga, kuwafanyia uharibifu wa vifaaa na kuwapokonya mali zao kama simu za mikononi. 

"Mimi ni mmoja wapo kati ya niliyevamiwa na watu waliokuwa wakidai ni polisi jamii studio kwa S2Kizzy na kupigwa bila hatia, kuumizwa na kuibiwa" amesema Hanstone 

Tukio hilo la kuvamiwa kwa Producer S2Kizzy akiwa studio kwake zimetoka asubuhi ya leo Oktoba 15, baada ya kufahamisha kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alieleza kuwa amepigwa na kuharibiwa vifaa vyake vya studio.