Hamisa Mobetto na Rayvanny waachiliwa kwa dhamana

Jumatano , 17th Feb , 2021

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni ACP Japhet Kibona, amesema ni kweli  wasanii Hamisa Mobetto na Rayvanny walikuwa wanashikiliwa na polisi kituo cha Osterbay lakini wameachiwa kwa dhamana na uchunguzi bado unaendelea kufanyika.

Msanii Rayvanny na Hamisa Mobetto

Akizungumzia hilo kupitia EATV & EA Radio Digital Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni ACP Japhet Kibona ameeleza kuwa

"Ni kweli walikamatwa jana, hii ni kesi ya polisi na hupaswi kueleza walichokizungumza ni nini ila kilichopo ni kusambaza picha kwenye mtandao bila ridhaa ya mmoja wapo mwenye hizo picha, Hamisa na Rayvanny walidhaminiwa wote".

"Tunaendelea na uchunguzi kwa kilichofanyika na uchunguzi wetu na upelelezi ndio utakaoridhia, pia kuna Mwanasheria ambaye atapitia kama kilichofanyika ni kosa la kijinai au la" ameongeza 

Rayvanny anadaiwa kuvujisha video mitandaoni akiwa ana-kiss na mtoto wa staa wa filamu Kajala Masanja ambaye ni mwanafunzi Paulah Kajala, na Hamisa Mobetto anadaiwa ndiyo alimpeleka mtoto huyo kwa Rayvanny.