Hamis afunguka kutaka Pesa kujiunga Konde Gang

Jumamosi , 12th Sep , 2020

Msanii aliyejipatia umaarufu kwenye mashindano kusaka vipaji vya kuimba Hamis BSS, amekata mzizi wa fitna ambao ulikuwa unadai alihitaji pesa nyingi ili kujiunga Konde Gang baada ya msanii Harmonize kuonyesha nia ya kutaka kumsaidia.

Msanii Hamis maarufu kama Hamis wa BSS

Akifunguka hilo kwenye show ya Friday Night Live ya East Africa Tv, Hamis BSS amesema si kweli kwamba alihitaji pesa nyingi ili kujiunga Konde Gang, pia amefurahi kuona wasanii wengine walivyotambulishwa Konde Gang bila ya hata yeye kuwepo.

"Si kweli kwamba nilihitaji pesa nyingi  kujiunga na Konde Gang, ila ni riziki tu Mungu anatoa kwa kila mtu, mimi kiukweli nimefurahi kwa wasanii waliotambulishwa, Naamini Mungu tu anafanikisha kwa kila mtu kwa wakati wake ila kwa kawaida natamani ningekuwa mimi" amesema Hamis wa BSS