Jumanne , 23rd Mei , 2017

Rapa Young Dee a.k.a Pakarasta mwenye hit song ya 'Bongo bahati mbaya' amekuwa na mtazamo tofauti na wenzake katika 'industry' ya muziki kwa kudai hakuna ushindani wowote kwa sasa japokuwa waimbaji wamekuwa ni wengi.

Young Dee ametoa kauli hiyo baada ya watu wengi kuwarushia lawama ma-producer kwa kusema wao ndiyo wanasababisha kufanya muziki wa sasa kutokuwa na ushindani katika 'game' na kusema kuwa  wasanii wengi wanaimba nyimbo ambazo hazina mashairi mazuri na kufanya nyimbo hizo kutofika mbali.

"Hamna ushindani kabisa sasa hivi kwenye muziki wa bongo fleva....Sasa hivi zinatoka nyimbo 20, unapita wimbo mmoja unasema kuna ushindani ?...Inatakiwa ukisema kwenye ushindani nyimbo 20 kama tano zinakimbizana ambazo unaweza kusema kuna ushindani...Watu wamerelax sana, muziki una watu wengi ila hakuna ushindani". Alisema Young Dee

Hata hivyo kauli hiyo ya Young Dee inafananishwa na ile aliyoitoa msanii  mkongwe,Makamua kwa kusema 'game' ya sasa imekuwa kama ‘buble gum’ kulingana na wanachokifanya wasanii wengi kwenye game.