Alhamisi , 11th Nov , 2021

Aliyekuwa Mtangazaji wa kipindi cha Lovers Rock ya East Africa Radio Baba T, amefariki dunia leo katika Hospitali ya Rabininsia iliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

Picha ya aliyekuwa mtangazaji wa Lovers Rock ya East Africa Radio

Rafiki wa karibu na marehemu Baba T, Gota Irie amesema taarifa zaidi kuhusu taratibu za mazishi zitatolewa kwa sasa wanasubiriwa ndugu zake kutoka nje ya nchi.

Zaidi msikie hapa akizungumzia chanzo cha kifo cha Baba T.