Jumanne , 28th Dec , 2021

Kutoka 254 Kenya mchekeshaji Eric Omondi anasema kwa Afrika Mashariki Diamond Platnumz ndio msanii anayemtambua na anastahili kupewa sifa hizo.

Picha ya Eric Omondi na Diamond Platnumz

Kupitia post yake ya Instagram inasema kuwa wasanii wa Kenya wamelala, Tanzania wamepoteza kwenye Amapiano, na Uganda wameacha kuimba hawajaribu tena.

"Wizkid alijaza 02 Arena siku 3 na Chris Brown alikuwepo, Burna Boy anashinda Grammys kila mwaka, Kenya wanaowasilisha kwenye Michezo ya Olimpiki ya muziki wa Kiafrika na mwanafunzi wa kidato cha pili mwenye miaka 14".

"Mwanamuziki Pekee wa Afrika Mashariki ninayemkubali ni Diamond Platnumz (Tumpe sifa pale anapostahili Chibu anajaribu), Sauti sol wanajaribu lakini haitoshi"

Erick Omond ame-make headline mitandaoni siku ya jana baada ya kusema Amapiano umeua muziki wa BongoFlava.