Dullvani afunguka sababu ya kuvaa madera 

Jumamosi , 2nd Jan , 2021

Mchekeshaji aliyejipatia umaarufu mitandaoni kwa kuigiza kama mwanamke na kuvaa madera Dullvani amesema aliamua kuja na 'style' hiyo kwa sababu waigizaji wengi wa vichekesho ni wanaume na wanawake wapo wachache.

Mchekeshaji Dullvani

Akipiga stori hizo kwenye show ya Firday Night Live ya East Africa TV ambayo inaruka kila siku ya Ijumaa kuanzia 3:00 mpaka 5:00 usiku Dullvani amesema 

"Uhusika ambao ulinitoa sehemu moja hadi sehemu kubwa zaidi ni ile ya Mama Chogo, japo wakati naanza watu walikuwa wanazungumzia vibaya, sasa hivi maneno yapo lakini yamepungua kwa kiasi kikubwa

"Mimi ni mwanaume sasa nikiigiza uhusika wa mwanaume haitakuwa haijakaa sawa kwa sababu tuna waigizaji wengi wa kiume lakini hatuna waigizaji wengi wa kike kwahiyo ndiyo maana nikaja na wazo la kuigiza kama mwanamke" ameongeza 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.