"Cheni zangu za minyororo ni dola 10000" Harmorapa

Jumamosi , 10th Oct , 2020

Msanii Harmorapa amesema cheni zake za minyororo zina thamani ya dola 10000 sawa na milioni 23 za kitanzania, japo huwa hapendi kutaja gharama hizo kwa sababu watu hawawezi kuamini.

Msanii Harmorapa

Akisema hilo kwenye show ya Friday Night Live ya East Africa TV msanii huyo ambaye kwa sasa ana muonekano mpya kuanzia kunyoa mtindo wa para, kuvaa cheni za minyororo na hereni amesema kuwa 

"Hii cheni mimi mwenyewe hata sielewi nimejikuta tu inatokea, ukisema nimerudi ukoloni hapana wala sikuwepo kipindi cha ukoloni kwanza enzi za ukoloni sijakuwepo, thamani yake ni dola 10000 japo sipendagi kwa sababu watu hawawezi kuamini

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.