Chanzo cha Harmorapa kumwaga machozi kisa Alikiba

Jumanne , 30th Mar , 2021

Ni 'Headlines' za msanii wa BongoFleva Harmorapa ambaye amesema kukutana na Alikiba imekuwa kama ndoto kwake na ilimfanya atoe machozi kwa sababu hakuamini kama Alikiba ni shabiki yake na anamfuatilia.

Msanii Alikiba upande wa kushoto, kulia ni Harmorapa

"Niliona kama ndoto kukutana na brother Alikiba, dunia inamtambua kama mfalme wa muziki Africa, huyu jamaa ni mtu poa sana tofauti na watu wanavyomchukulia, ana nidhamu, heshima na upendo wa kweli kwa kila mmoja bila kubagua we niwa dizaini gani" amesema Harmorapa

"Alivyoingia 'backstage' tulipo kuwa tumekaa wasanii alikuja nilipokaa mimi, alivyofika alinikumbatia na kufurah sana kukutana na mimi, basi tukaanza kutaniana na kucheka na mbele ya story aliniambia ananikubali sana"

"Aliishangaza alipoimba mistari ya wimbo wangu, nilianza kulia sikuamini mwisho wa  picha aliniambia nataka wanaokudharau na kukuchukulia poa wakuheshimu, nikamuhoji why unasema hivyo akanijibu nataka nikubariki kwa kukupigia chorus kwenye wimbo wako mmoja" ameongeza 

Alikiba na Harmorapa walikutana siku ya mwisho ya kuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli huko Wilayani Chato, Mkoani Geita.

Zaidi tazama hapa kwenye video.