Jumanne , 24th Nov , 2020

Msanii Bushoke amesema hajalikimbia Jiji la Dar Es Salaam kwa sababu ya ushindani bali kuna kelele nyingi na yeye hapendi kelele hivyo anahitaji muda wa kupumzika na hapendi kuongeaongea.

Msanii Bushoke Ruta

Akizungumza na e-Newz ya East Africa TV  msanii huyo ambaye kwa sasa anaishi Jijini Dodoma amesema kuwa 

"Hakuna ushindani wowote kuna kelele nyingi halafu wengine hatupendi kelele tunahitaji muda wa kupumzika, kwa anayesema nimekimbia Dar Es Salaam atakuwa hajui kuchambua mambo vizuri na mimi sipendi sana kuongeaongea" amesema Bushoke

"Dodoma sasa hivi limeshakuwa Jiji sio kama kijiji kwamba useme amekimbilia Dodoma, huku kila msanii anakuja kwa hiyo kwa msanii yeyote ambaye anahisi nimekimbia atakuja huku halafu ataona kama kweli nimekimbia au nimekuja kupunga upepo" ameongeza 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video