Ben Pol aongea yote kuhusu kubadili dini

Jumapili , 10th Jan , 2021

Kupitia Friday Night Live msanii Ben Pol  ameweka wazi kuhusu zile picha zilizosambaa zikimwonesha amebadili dini kutoka kuwa Mkristo na kuwa Muislamu.

Msanii Ben Pol (katikati).

Ben Pol amesema kuwa suala la dini analiacha kwa wale tu ambao watakutana naye kwenye nyumba ya kuabudi ili lisije likachanganya mashabiki zake.

'Unajua wakati naanza muziki nilikuwa huru na mtu wa kila mtu ndio maana nataka iendelee kuwa hivyo masuala yangu binafasi kama dini sitaki sana kuyaongelea na hata picha zilivyotoka nikasema sitafafanua lolote ila tu kuna watu nitakutana nao kwenye nyumba ya kuabudu'', amesema.

Tazama Video hapo chini akiongea zaidi