Barnaba ajibu kejeli za mama mtoto wake

Sunday , 13th Aug , 2017

Mwanamuziki anayesumbua kwa sasa na ngoma ya 'Tunafanana' Barnaba Elias 'Barnaba Classic' ametupa jiwe gizani linalodaiwa kuwa ni dongo kwa mzazi mwenzake baada ya kufunguka kwenye mtandao kuwa kumtukana mwanamke ni sawa na kumtukana mzazi wake.

Msanii Barnaba Classic

Dongo hilo Barnaba ameliweka kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya mzazi mwenzke huyo kudai kuwa baada ya miaka mtano kupita hatimaye sasa amefanikiwa kupata amani ya moyo ambayo ndicho kitu alichokuwa akikikosa kwa muda wote.

Barnaba ameandika "Mama aliniambia ukimtukana mwanamke basi umenitukana na mimi. Siku zote nawaona kama mama zangu hongera wanawake wote duniani Salamu zangu juu yenu Jumapili ya leo nawapenda Sana"

 

Ujumbe wa Barnaba aliouweka Instagram leo hii baada ya ujumbe wa Mzazi mwenzake

Mzazi mwenzake Barnaba, Zuu Namela ambaye walibahatika kupata mtoto wa kiume 'Steve' leo asubuhi aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kisha kufuta ujumbe huu.

"Ni watu wachache sana wanaojua nikitu gani nilikua nakosa katika maisha yangu! Unaweza ukapata kila kitu kwenye maisha ila ukakosa furaha,amani,heshima......kwa zaidi ya miaka mitano hichi ndo nilicho kuwa nakitafuta #AMANIYAMOYO " 

Ujumbe wa mzazi mwenzake Barnaba, Bi Zuu Namela kabla ya kuufuta.

Recent Posts

Current Affairs
Rais Mugabe atumbuliwa

Msanii Irene Uwoya.

Current Affairs
Uwoya otokwa povu kisa mtoto

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi.

Current Affairs
Serikali kuvunja nyumba zilizojengwa bila kibali