Barakah The Prince afunguka kuhusu kutumia Uganga

Alhamisi , 24th Sep , 2020

Msanii wa BongoFleva na mkali wa nyimbo za mapenzi Baraka The  Prince, amefunguka kuhusu suala zima la wasanii kujihusisha na mambo ya kishirikina katika muziki wao kama njia moja wapo ya kutaka kufanikiwa au kutoboa kwenye muziki.

Msanii wa BongoFleva Barakah The Prince

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital amesema kuwa kwa upande wake hana imani na mambo ya kishirikina na anamuamini Mungu kama mganga wake mkuu katika muziki.

Siamini sana mambo ya ushirikina na sijawahi kufanya nasikiaga tu watu wanasema  ila nimeweza kufanikiwa bila kwenda kwa waganga mimi mganga wangu mkuu ni Mungu mwanadamu mwenzangu atawezaje kunifungulia mambo naamini sana katika sala na Mungu” amesema Baraka The Prince