Anjella apelekwa mjini kwa Kiingereza

Jumapili , 14th Feb , 2021

Msanii wa Bongofleva Harmonize, amesherehekea siku ya Valentine kwa kuachia ngoma yake mpya #AllNight aliyomshirikisha msanii chipukizi Anjella.

Anjella na Harmonize

Harmonize ametimiza ahadi yake kwa Anjella kuwa atampeleka mjini, mara tu baada ya kuona clip zake akiimba na kuvutiwa na kipaji chake.

Katika ngoma hiyo Anjella ameimba chorus na lugha iliyotumika kwa kiasi kikubwa ni Kiingereza. Kwa mujibu wa Harmonize, hii ndio single yake ya kwanza official kuitoa kwa mwaka 2021.

Harmonize ameanza na audio na huenda akaachia video ya ngoma hiyo muda si mrefu, kwani tayari alishadokeza kuwa ipo tayari muda mrefu.