Anjella aelezea Ugonjwa wa ajabu unaomsumbua

Jumamosi , 20th Feb , 2021

Msanii anayesaidiwa na Harmonize kwenye upande wa muziki na matibabu, Anjella ameeleza kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa miguu ambao ulimuanza tangu akiwa darasa la 7.

Msanii Anjella ndani ya studio za East Africa Radio.

Anjella amesema amepambana sana na ugonjwa huo mpaka wakakata tamaa wakabaki kufanya maombi ila anamshukuru Harmonize ambaye ameahidi atamsaidia na kumpeleka nchini India.

"Tatizo la miguu lilianza nikiwa darasa 7 sasa imepita miaka 8, nililala na nilivyoamka mguu ukawa unauma, tukakaa kama wiki ukaanza kutoa uvimbe, tukaenda Hospitali ya kwanza Ugonjwa hakuonekana ,ya pili wakasema ni tende, ya tatu wakasema mirija inayopitisha uchafu imeziba"

"Tukapambana na matibabu hadi tukapoteza matumaini, namshukuru Mungu ameniletea Harmonize ambaye amesema atanibitia na atanitafutia Hospitali za hapa wanaoweza kushughulikia tatizo langu na ikishindikana atanipeleka India" ameongeza Anjella 

Zaidi mtazame hapa chini kwenye video