Ijumaa , 25th Sep , 2020

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuhukumu msanii Rutyfiya Abubakary maarufu kama 'Amber Rutty' mumewe Said Bakary na James Charles 'James Delicious' kulipa faini ya Mil. 11 ama jela miaka 5 baada ya kutiwa hatiani kwa makosa manne ikiwemo kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Kutoka kushoto ni James Charles, mume wa Amber Rutty Said Bakary na Amber Rutty mwenyewe

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya baada ya mahakama hiyo kujiridhisha pasina kuacha ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.

"Nimezingatia hoja za pande zote mbili na athari za makosa haya, ni kweli washitakiwa wote vijana na wanategemewa, nimeona mshitakiwa wa kwanza anajutia, kutokana na mazingira ya kesi hii adhabu yake ni miaka 30 kila kosa ambapo nikiwafunga mtapotea kabisa" amesema Hakimu Mkazi Mfawidhi Godfrey Isaya 

"Hivyo kwa mazingira mliyoyasema na lengo la adhabu ni kujirudi, mshitakiwa wa kwanza utalipa Milioni 3 ama jela miaka 5 (Amber Rutty)  mshitakiwa wa pili utalipa faini ya milioni 3 ama jela miaka 5 (Said Bakary )  na mshitakiwa wa tatu faini milioni 5 ama jela miaka 5 (James Charles) na adhabu zitaenda sambamba" ameongeza 

Kwa sasa washtakiwa wote wako mahabusu hadi hapo watakapolipa faini hizo