Jumatatu , 29th Mar , 2021

Mtunga mashairi ya viongozi Mzee Msafiri Himba amemtungia shairi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ikiwa ni ishara ya kumpongeza kwa kuwa Rais wa kwanza mwanamke kwenye historia ya Tanzania.

Upande wa kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, kushoto ni Mzee Msafiri Himba

Mzee Himba amesema shairi hilo linaitwa 'Samia Mjengoni' na ilitumia dakika 30 mpaka 35 kukamilisha utunzi wa shairi na alilitunga akiwa ndani ya gari wakati anaelekea Mkuranga.

Mtunzi huyo wa mashairi ameendelea kusema dhumuni la kumtungia Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan shairi hilo ni kuwaondoa hofu watanzania juu ya uwezo wake kwenye uongozi kwani anajiamini, anajielewa na anajua kutenda wajibu wake ipasavyo.

Aidha amesema ametunga mashairi mengi ya kuwasifu viongozi na mengine ya yanayohusu viongozi waliofariki kama Rais wa kwanza wa Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Awamu ya tatu Hayati Benjamin William Mkapa.

Zaidi mtazame hapa chini akilisoma shairi hilo.