Alikiba apewa tahadhari nzito kwenye mgahawa

Ijumaa , 25th Sep , 2020

Staa wa BongoFleva Alikiba amesema siku ya jana alipigiwa simu ya kupewa tahadhari ya kutokwenda kula kwenye mgahawa mmoja uliopo mitaa ya Upanga baada ya 'cashier' wa mgahawa huo kumsema vibaya.

Msanii wa BongoFleva Alikiba

Alikiba amesema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio mara baada ya kuulizwa kwanini ametoa wimbo wa aina hiyo wakati hawamjazoea akifanya miziki ya aina hiyo. 

"Muziki una season na mimi nnimeona huu ndiyo wakati wake nilisemaga nikianza kujibu mtashangaa maana tukipiga kelele tutakuwa wote wajinga halafu hatutasikilizana ila baadaye nikitulia nitakupa jibu lako na sipo kwa ajili ya ushindani

"Baada ya kuachia hii ngoma nilienda mahali kula mitaa ya Upanga ambapo watu wanaouza hapo nawafahamu, sasa kuna kijana mmoja ni cashier  pale, baada ya kula wakati naondoka akawa ananiongelea vibaya sana hadi nikapigiwa simu kupewa tahadhari nisiende kula tena pale, maana naweza kuekewa hadi sumu kwa jinsi ambavyo alikuwa ananiongelea, najua watu hawanipendi lakini mimi sijali" ameongeza