Jumatano , 29th Dec , 2021

Staa wa muziki Bongo Alikiba amemjibu Maua Sama kwa kumwambia hakuna mtu wa kumpiga akirudia kusikiliza wimbo wake wa Zai, Utu ya Alikiba na I wish ya Kusah.

Picha ya msanii Alikiba na Maua Sama

Kupitia ukarasa wa Twitter Maua Sama ameandika kwamba "Kwani ikitokea hujaimba Amapiano unaweza kufutiwa cheti cha usajili BASATA au utapokonywa NIDA & Passport?"

"Nipo zangu sehemu hapa nakunywa soda nasikiliza Zai, Utu & I wish (On Repeat) nipo Airport njooni mnipige"

Alikiba akacomment kwenye tweet hiyo kwa kuandika "Hakuna wa kukupiga Zai wangu".