Alichokisema Stamina kuhusu Prof Jay

Alhamisi , 19th Nov , 2020

MwanaHipHop Stamina Shorwebwenzi amesema msanii na mwanasiasa Prof Jay anatakiwa heshima ya kipekee kwani amekuwa na ushawishi kwa wasanii wengine pia alibadilisha akili za wazee ambao walikuwa wanaamini muziki ni uhuni

Msanii Stamina upande wa kulia, kushoto ni Prof Jay

Stamina amesema hakuna msanii wa sasa ambaye hajamsikiliza Prof Jay wakati anakuwa au akijiandaa kuingia kwenye muziki pia ameipambania 'game' ya BongoFleva mpaka kufikia hapa.

"Prof Jay ni kaka yangu au baba ana nafasi hiyo kwangu, kuna muda nikipiga naye stori namwambia simuoni kama mpinzani ila namuona kitaifa zaidi ila tunatakiwa kuheshimu maamuzi na maisha lazima yaendelee, nimefika hadi studio za Mwanalizombe Mikumi na nina ngoma naye

"Hakuna rapa yeyote ambaye hajawahi kumsikiliza Prof Jay, ni mmoja kati ya inspiration  kubwa kwa watu pia alibadilisha akili za wazee wetu kwamba muziki sio uhuni,kwenye maisha muogope sana mtu anayepambania watu wengine" ameongeza

Prof Jay ni mmoja kati ya wasanii wa kwanza na wenye heshima kwa kuanza muziki hapa nchini Tanzania ambapo amefanikiwa kutengeneza ngoma kali ambazo zilifanya vizuri kwenye 'chart' na kubeba tuzo mbalimbali.