Alichofanyiwa Nyoshi kwenye uongozi wa Magufuli

Jumamosi , 27th Mar , 2021

Raia wa nchi ya Congo DR ambaye ni msanii anayefanya shughuli zake za kimuziki hapa Tanzania Nyoshi El Sadaat amesema tangu Hayati Dkt John Pombe Magufuli alivyoingia madarakani hakusumbuliwa kuhusu ishu ya makazi.

Kulia ni aliyekuwa Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli na msanii Nyoshi El Sadaat

Nyoshi El Sadaat amesema Dkt John Pombe Magufuli aliwafanya wageni wote waishio Tanzania kuwa salama, uhuru na hawajasumbuliwa kwa chochote ndio maana mataifa wengine walitamani wapate kiongozi kama yeye.

"Naishi hapa kwa kibali lakini tangu ameingia madarakani sijaona mtu anakuja kunisumbua nyumbani kuhusu kibali changu, aliwawekea wageni uhuru wa kuishi vizuri na kwa miaka yake ytoe wageni tumekaa kwa salama, pia ameleta maendeleo ya hapa ndio maana mataifa mengine walitamani kuwa na Rais kama yeye" amesema Nyoshi El Sadaat 

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt John Pombe Magufuli umezikwa siku ya jana Machi 26 nyumbani kwao Chato Mkoani Geita.

Zaidi mtazame hapa chini.