Jumanne , 5th Jan , 2021

Leo ni Januari 5, kumbukumbu ya kuzaliwa kwa aliyekuwa msanii wa HipHop Golden Jacob 'Godzillah' ambaye alifariki dunia siku ya Februari 12,2019 ambapo kama angelikuwa hai angesheherekea kutimiza umri wa miaka miaka 32.

Msanii Mwasiti akiwa na Godzillah enzi za uhai wake

Huyu hapa ni dada mkuu wa Bongoleva pia alikuwa mtu wa karibu na marehemu Godzillah, Mwasiti ameshea stori kuhusu kitu alichoambiwa na mama mzazi wa aliyeuwa msanii huyo.

"Nilimjua Zilla wakati ana-hit na wimbo wake wa salasala, muunganiko wetu ulikuja baada ya kukutana na mama yake ambaye aliniomba nimuangalie Godzilla nikasema sawa, tulikuwa marafiki, mtu na dada yake na alikuwa anapenda kuniita Dada Chitty" amesema Mwasiti 

"Zillah alikuwa mtu mwenye huruma sana tofauti na watu walivyokuwa wanamuona mitandaoni, alikuwa ana uthubutu sana, vizazi vinavyokuja wajifunze kutoka kwake vinaweza kuwasogeza kwenye carrier ya wanaotaka ku-rap na wanaopenda muziki" ameongeza 

Mwasiti na Godzillah wamewahi kufanya kazi kwa pamoja ambazo zimefanya vizuri kwenye muziki wa BongoFlava kama Soldier na First class.