Alhamisi , 30th Oct , 2014

Msanii wa muziki AK47, ametoa ushauri mzito kwa kaka yake Jose Chameleone kujikita studio na kutengeneza muziki mzuri zaidi, na kuacha kutumia nguvu kuwalazimisha Ma-DJ kucheza muziki wake.

Jose Chameleone, AK47

Kauli hii ya AK47 imekuja baada ya ripoti za kaka yake huyu kumletea fujo Dj wa klabu maarufu huko Kampala Uganda, kwa kutokupiga ngoma yake maarufu ya Wale Wale katika 'playlist' yake.

AK47 amesema kuwa, kwa ufahamu wake, ma-DJ wote huwa na jukumu la kucheza muziki mzuri kwa ajili ya kuwaridhisha mashabiki wa muziki huu, na si kazi yao kucheza muziki kwa ajili ya kuwafurahisha wasanii ambao ndio wanaozifanya rekodi hizi.