Jumamosi , 16th Aug , 2014

Msanii Weasel kutoka Uganda, amepata baraka zote kutoka kwa AK47 katika mchakato wa kuhalalisha penzi lake na mwanadada Samira ambaye ambaye yeye AK47 mwenyewe aliwahi kuwa na mahusiano naye kipindi cha nyuma.

AK47, Weasel na Samira

AK47 ameweka ujumbe wake mtandaoni kutoa hongera kwa kaka yake ambaye amejitambulisha kwa wazazi wa Samira hivi juzi, na kusema kuwa anawatakia maisha mema.

Samira kwa sasa tayari ana Ujauzito wa miezi mitano wa Weasel, na wawili hawa wanatarajia kufunga ndoa siku za usoni.