Agness amkana Uchebe hadharani "Alikuwa na Stress"

Alhamisi , 18th Feb , 2021

Msanii na mfanyabiashara Official Agness amesema hakuwahi kuwa kwenye mahusiano na Uchebe bali alitumika kujifanya wapo kwenye mahusiano ili kumuumiza aliyekuwa mke wake Shilole baada ya kuachana kwao.

Picha ya Uchebe na Official Agness

Akifichua siri hiyo Agness wa Uchebe amesema kilichoendelea kati yao ni urafiki tu japo nje walijulikana kama wapenzi, ila ukweli ni kwamba wanaheshimiana kama kaka na dada na hawakuwahi kushea kitanda kimoja.

"Mimi na Uchebe hatujawahi kuwa na mahusiano alikuwa ni rafiki yangu wa kawaida ila kulikuwa na drama zinaendelea, Uchebe alikuwa na stress baada ya kuchana na mkewe hivyo akanipanga kunitumia ili kumuumiza Shilole" amesema Agness wa Uchebe 

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.