20 Percent akasirishwa na Alikiba na Harmonize

Jumanne , 23rd Feb , 2021

Msanii 20 Percent amefunguka kusema anakasirishwa na tabia ya kuulizwa maswali yanayowahusu wasanii Alikiba na Harmonize kwa sababu sio kitu muhimu kwake na mashabiki zake.

Kushoto ni msanii 20 Percent, kulia ni Harmonize picha ndogo ni Alikiba

Akifunguka hilo kupitia EATV & EA Radio Digital msanii 20 Percent amesema kuwa 

"Nakasirishwa kuongeleshwa mambo mengi yasiyonihusu hata kama nikija na kazi zangu mkononi nitaulizwa kuhusu fulani na fulani, kwa mfano unaulizwa kuhusu Alikiba au Harmonize kitu ambacho pengine sio muhimu kwa mashabiki zangu ambao wanataka kujua kwa wakati huo, ni watu ambao wamekaa kwenye mazingira ya kiki na mashindano ya mitandaoni

Zaidi bonyeza hapa chini kumtazama