Ijumaa , 24th Sep , 2021

Msanii na bosi wa Konde Music Worldwide, Harmonize ametangaza kusogeza mbele siku (Cheed Day) ya kuachia kazi ya kwanza kutoka kwa msanii wa lebo hiyo Cheed.

Picha ya Msanii Cheed

Jeshi ametangaza hilo kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa hakutokuwa na Cheed Day leo kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao.

"Siku zote mwenye subira bila shaka yupo karibu na Mungu, najua kwa kiasi gani mnamsubiri Cheed ila ningependa kuchukua nafasi hii kuwataarifu kwamba kwa sababu zilizopo kando ya uwezo wetu, Cheed Day haitokuwepo tarehe 24/09/2021 kama tulivyopanga hapo awali, tunawaahidi kuwajuza lini na siku gani hivi punde" - ameandika Harmonize