Jumapili , 18th Oct , 2020

Wasimamizi wa uchaguzi wameshauriwa kurudia tena kusoma maelekezo yaliyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili kujikumbusha taratibu zote za mchakato wa uchaguzi.

Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera

Akizungumza leo Oktoba 18, 2020 katika mkutano uliowakutanisha waratibu na wasimamizi wa uchaguzi, Mkurugenzi wa Uchaguzi Dkt. Wilson Mahera, amesema kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kutasababisha malalamiko na kupelekea uvunjifu wa amani.

''Kuna mambo muhimu ya kuzingatia yatawasaidieni kuboresha utendaji kazi wenu katika kuendesha uchaguzi kwa weledi na ufanisi zaidi'',  amesema Dkt. Mahera

Aidha baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi wamesema wamepokea maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wameahidi kwenda kuyafanyia kazi ambapo pia wamewataka wananchi  kupiga kura bila kuwa na hofu yoyote.