Mapya ya CUF kuhusu Maalim Seif

Jumapili , 24th Jan , 2021

Chama cha wananchi (CUF) kimekanusha taarifa zinazosambaa zikidai kuwa chama hicho kimesambaratika na kufa ilihali bado wanachama wa chama hicho wapo wakiendelea na majukumu ya kukijenga chama.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee CUF, Mohamed Chunga.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 24, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazee CUF, Mohamed Chunga, amesema madai kuwa Maalim Seif Hamad amesambaratisha chama hiko ni ya uongo kwani Maalim sio muasisi wa chama na hana uwezo  wa kusambaratisha huku akiwataka wanachama sambamba na watanzania kupuuza taarifa hizo. 

"Sisi Chama Cha Wananchi, CUF - Wazee, taarifa hizo ni za uzushi na hazina maana yeyote kwasababu chama ni watu na wanachama, na wanachama wa CUF wapo na hata uchaguzi ulipofanywa bado tuna wabunge wawili tumewapata sasa anaposema chama kimekufa tunashangaa" amesema Mzee Chunga

Aidha Mohamed Chunga amesema wataendelea kuhamasisha na kulinda amani na utulivu nchini pamoja na kuimaraisha chama chao huku wakizingatia misingi iliyowekwa katika kuendeleza na kudumisha demokrasia nchini.