Jumapili , 7th Feb , 2021

Serikali kupitia Wizara ya Afya imepitisha dawa tano tofauti za asili zitakazotumika kujikinga na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi

Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi, ameyabainisha hayo Jijini Dodoma ambapo amesema Serikali imeweka mkakati wa kupatikana dawa asili katika vituo vya kutolea huduma za afya na maduka ya dawa za binadamu ambazo zitakua zimepitishwa na mkemia mkuu wa serikali.

Mkurugenzi Msaidizi Tiba Asili kutoka Wizara ya Afya,  Dkt. Paul Mhame, amesema serikali kupitia Taasisi zake imeweza kuchambua na kuidhinisha dawa za kunywa aina 5 na dawa aina 4 za  mafuta tete kwa ajili ya kujifukiza ambazo zimekidhidi vigezo kuweza kutumika kwa binadamu na dawa hizo za kunywa ni NIMRICAF, COVIDOL, BINGWA, PLANET ++ pamoja na COVOTANZA huku zile za mafuta tete zikiwa ni BUPIJI pamoja na UZIMA. 

Kwa upande wake DK. Otieno kutoka Taasisi ya Tiba Asilia Muhimbili amesisitiza umuhimu wa wananchi kuacha kuchanganya dawa zaidi ya moja kwa wakati mmoja wakati wa kutumia. Amesema ni vema pia wananchi wafuate maelekezo sahihi ya matumizi ya hizi dawa na kuzingatia usalama wake.