Zitto agonga mwamba urais TFF

Monday , 19th Jun , 2017

Mbio za kugombea urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) zimegonga mwamba kwa Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Zitto Zuberi Kabwe kwa kile alichodai kuwa atashindwa kuzitumikia kofia tatu kwa wakati mmoja.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe

Zitto amebainisha hayo baada ya kupokea maombi kwa baadhi ya watu mbalimbali wakiwemo viongozi wakubwa wakimtaka akachukue fomu ya Urais TFF pindi dirisha likifunguliwa ili aweze kugombea nafasi hiyo hapo awali.

"Nimetafakari na kuchukua uamuzi kwamba uongozi wa ACT- Wazalendo na Ubunge ni nafasi ambazo ninazo tayari, wakati Urais TFF ni nafasi mpya. Kwa hali hiyo na kwa mapenzi makubwa ya soka la Tanzania, nimeamua nisichukue fomu ya kugombea Urais TFF kwani naweza kuomba kazi ambayo nitashindwa kuitumikia kwa muda wa kutosha kutokana na majukumu yangu kwenye chama na Ubunge" aliandika Zitto kupitia ukurasa wake wa facebook.

Aidha, Zitto ameendelea kwa kusema uamuzi wake umezingatia umezingatia mapenzi makubwa ya kwa soka la Tanzania.

" Nikijitokeza kuwania Urais wa TFF leo halafu nikakosa muda mzuri wa kutimiza matarajio ya wapenda soka nchini, utakuwa ni usaliti mkubwa kwa maendeleo ya soka la Tanzania" alisisitiza Zitto.

Huu ndiyo ujumbe wa Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake.

Recent Posts

Mkongwe TID

Entertainment
TID ataka wakongwe wathaminiwe

Riyama Ally akiwa na mumewe Haji Mwalimu Mzee 'Leo Mysterio'.

Entertainment
Niachieni mume wangu, sie twazidi kupendana!

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Simon Sirro

Current Affairs
Sirro aahidi amani siku ya Eid

Msanii wa Bongo fleva, Foby

Entertainment
Foby amtamani Ben Pol
Entertainment
Nay akomaa na Msodoki