Jumatano , 16th Sep , 2020

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), imeyaruhusu makampuni ya Ndege za Kenya yaliyokuwa yamefungiwa kufanya shughuli zake nchini kuendelea hii ni baada ya Kenya kuondoa zuio la Watanzania, kuwekwa karantini wanapowasili nchini humo.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari

Taarifa hiyo imetolewa leo Septemba 16, 2020, na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Hamza Johari, ambapo amesema kuwa tamko hilo linakuja baada baada ya Serikali ya Kenya kuiondolea Tanzania vikwazo vya raia wake kuingia humo bila kuwekwa karanyini.

Aidha  Mkurugenzi huyo ameyataja mashirika ya Ndege ya Kenya yaliyoruhusiwa kuendelea na shughuli zake kuwa ni  Kenya Airways, Fly 540 Limited, Safarilink Aviation na AirKenya Express Limited.

Jana Septemba 15, 2020, nchi ya Kenya ilitoa orodha ya nchi 147 ambazo raia wake wataingia nchini humo bila kuwekwa karantini na katika nchi hizo Tanzania iliorodheshwa.