Jumatatu , 21st Sep , 2020

Rais wa Serikali ya Zanzibar Dk.  Ali Mohamed Shein ameweka wazi makusuidio ya serikali ya Zanzibar kuifanya Mbweni kuwa mji wa kisasa huku akisema visiwa hivyo vina historia kubwa.

Rais wa Zanzibar Dkt Ali Shein

Amesema hayo leo Septemba, 21, wakakti akihutubia wananchi na watumishi wa umma waliohudhuria ufunguzi wa nyumba za makazi mradi wa makazi Mbweni ulioandaliwana Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar(ZSSF) ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.

"Treni ilianza Zanzibar kabla ya Tanganyika wakati huo, kabla ya kenya kabla ya Uganda, Zanzibar ina historia kubwa na historia yake ya treni ni Mbweni tunadhamiria kuufanya Mbweni kuwa mji wa kisasa na ndio jitihada zetu hizi" amesema Dk.Shein.

Aidha Dk. Shein amefafanua  kuwa mradi huo wa nyumba za makazi ni jitihada za serikali ya Zanzibar katika kuimarisha sekta ya makazi.

"Nyumba hizi za makazi za hapa mbweni ambazo sie tunaziona wengine mara ya kwanza au wengine mara nyingi ni jitihada za serikali yetu ya mapinduzi ya Zanzibar za kuimarisha sekta ya makazi ila wananchi wapate mahali pazuri pakuishi" amesema Dk. shein