Jumatatu , 19th Mei , 2014

Wizara ya afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusiana na hali ya ugonjwa wa Dengue nchini na kwamba mpaka sasa ni wagonjwa 31 tu ndio wamelazwa katika hospitali mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Msemaji wa wizara ya afya na ustawi wa jamii, Nsachris Mwamwaja.

Msemaji wa wizara hiyo Nsachris Mwamwaja, ameiambia East Africa Radio kuwa tayari serikali imeingiza nchini vifaa kwa ajili ya kupimia ugonjwa huo huduma ambayo amesema inatolewa bure.

Kwa mujibu wa Mwamwaja, vifaa hivyo vimeingizwa nchini siku ya Ijumaa vikitokea nje ya nchi na kwamba vimeshasambazwa katika vituo vyote vya tiba hatua inayomaliza malalamiko yaliyokwepo awali kuwa vifaa hivyo ni adimu.