Jumatatu , 29th Sep , 2014

Watu wenye Ulemavu wa kusikia nchini Tanzania wameitaka Serikali kutulia mkazo kuweka miundo mbinu shughuli mbalimbali za kijamii ili kuweza kuwasiliana kwa urahisi.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto nchini Tanzania Bi. Sophia Simba.

Akizungumza Jijini Arusha Makamu mwenyekiti wa chama hicho Tanzania Marii Sosula amesema kuwa kundi lao linaonekana kutwengwa kutokana na kukosa watu watakoweza kuwalekeza hasa wanapokwenda kuapta huduma za afya na kwingine kwingine.

Aidha Sosula ametaka na vyombo vya habari hususani kwenye luninga kuweza kuweka wakalimani wa Lugha za alama kwenye Luninga ili kuweza kufatilia habari na pia kujua kinachoendelea na kuitaka Katiba ijayo itambue haki hiyo ya kupata habari.

Wakati huo huo, wanasayansi Nchini Kenya wanaamini kuwa chanjo mpya ya Ugonjwa wa Malaria itakua imepatika ifikapo mwaka ujao ambapo itatumika kumaliza ugonjwa huo nchini Kenya na katika mataifa ya jirani ikiwemo Tanzania.

Akizumgumza Jijini Nairobi Mtaalamu wa magonjwa nchini Kenya Prof. K.M Bhatt amesema chanjo hiyo imeshafanyiwa majaribio na itaanza kutumika rasmi mwaka ujao.

Chanjo hiyo RTS inasemekana kuwa uwezo wa kuzuia virusi vya ugonjwa huo kuingia katiia ini na kuzuia katika mishipa ya Damu kuathiri chembecheme nyekundu za damu na kusababisha Ugonjwa huo.