Jumatatu , 25th Jul , 2016

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Kassim, amewataka mawaziri ambao wananyumba na ofisi Dodoma wahamie haraka huku akimtaka Waziri Ofisi ya Waziri akamilishe nyumba yake mpaka mwezi wa tisa awe amehamia huko.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Kassim

Akizungumza leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa Mkoani Dodoma, Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa atatekeleza agizo hilo kwa kulisimamia kikamilifu ili kuhakikisha wizara zote zinahamia makao makuu hayo ya nchi.

Mhe. Majaliwa amesema kuwa Ifikapo mwezi wa tisa atazihamishia ofisi zake mkoani humo huku akisema kuwa mawaziri wengine hawanabudi kumfuata pindi tu atakapotekeleza jambo hilo baada ya nyumba yake kukamilika.

Pamoja na kutekeleza agizo hilo waziri Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwataka Wakazi, na Mamlaka husika za Mkoa wa Dodoma kuhakikisha huduma zote muhimu zinapatikana huku akiwataka wawekezaji kutumia fursa hiyo kuwekeza mkoani humo kutokana na wageni watakaokua wanazuru Mkoa huo.

Aidha Ameongeza kwa Wakazi wa Dodoma wahakikishe kuwa kisiwa cha Amani lakini pia amewataka wakazi kuwekeza katika maeneo mbalimbali ikiwemo kujenga Hoteli mbalimbali, Nyumba za kulala wageni na vitega uchumi vingine vya kujiingizia kipato.