Jumatatu , 20th Sep , 2021

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amegiza marumaru zilizowekwa kwenye sakafu ya wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Karagwe ziondolewe haraka kwani hazina viwango vinavyotakiwa na badala yake ziwekwe marumaru zenye ubora unaokidhi viwango vya serikali. 

Marumaru zilizowekwa kwenye wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya ya Karagwe

Waziri Mkuu Majaliwa, ametoa maagizo hayo wakati alipokagua ujenzi wa hospitali hiyo akiwa katika ziara yake mkoani Kagera.