Jumapili , 10th Jan , 2021

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene ameagiza maofisa watano wa polisi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kuchukuliwa hatua za kinidhamu baada ya intelijensia yake kubaini wanajihusisha na matukio ya ukiukwaji wa maadili.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene.

Simbachawene ametoa agizo hilo akiwa kwenye muendelezo wa ziara yake katika vikosi mbambali vya jeshi la polisi kanda ya Dar es salaam kwa ajili ya kukagua na kufanya tathmini ya utendaji kazi na kusema Serikali itaendelea kuwachukulia hatua za kinidhamu wanaochafua heshima ya jeshi hilo.

Nimewataja kwa majina na nimewakabidhi hawa viongozi na tutawachukulia hatua za kinidhamu kwa sababu tuna taarifa za kiintelijensia wanafanya vitendo hivyo ikiwamo kubabaisha abiria wakati wa kuondoka, wakiona abiria huyu ana uwezo wa kifedha wanafanya ubabaishaji,” amesema.

Simbachawene amesema licha ya kabainika kutumia nafasi zao kutapeli baadhi ya abiria maofisa hao wamebainika pia  wanajihusisha na mtandao wa kusafirisha mabinti kwenda kufanya kazi za ndani katika nchi za uarabuni .

Sambamba na hilo Simbachawene, ameagiza  taarifa zote za majanga ya moto na maokozi katika mikoa yote nchini zitolewe na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na siyo vyombo vingine vya ulinzi na usalama wala taasisi zingine.