Jumapili , 10th Jan , 2021

Naibu Waziri wa Tamisemi David Silinde ametaka hatua kali kuchukuliwa kwa wananchi waongoza migomo ya kutochangia shughuli za maendeleo au kuzuia miradi ya maendeleo inayopelekwa na serikali katika maeneo yao kwa faida ya watu wote wa eneo husika.

Naibu Waziri wa Tamisemi David Silinde.

Silinde amechukua uamuzi huo baada ya Wananchi wa kijiji cha Riroda kata ya Riroda wilaya ya Babati mkoani Manyara wakugomea mradi wa mabweni uliotolewa na Ofisi ya Rais TAMISEMI EP4R wakidai kuwa na harufu ya ufisadi kutoka kwa wanaokusanya michango katika kijiji chao kwani baadhi ya michango fedha zao zilipigwa na hakupewa taarifa ya mapato na matumizi.

Ufanyike uchunguzi kwa yeyote aliyekula fedha za michango ya wananchi achukuliwe hatua kali za kisheria bila upendeleo wowote kwa fedha zilizochangwa kwa ajili ya choo, wananchi kwa hiyari yao wachangie ujenzi wa mabweni ambao unaendelea kwasasa na kufikia sehemu ya upauaji na wakuu wa wilaya chukueni hatua ya kuwaweka ndani wananchi wanaoongoza migomo”, amesema Silinde.

Kwa upande wao viongozi wa Wilaya ya Babati Mkuu wa Wilaya LazaroTwange na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Babati John Nchimbi wasema walifanya jitihada sana ya kukaa nao meza moja wananchi wa kijiji hicho wakubali mradi huo kujengwa katika shule hiyo ili uweze saidia wanafunzi wanaotoka mbali kuweza kukaa shuleni kusoma vizuri.

Nao wananchi wa kijiji hicho wamesema waligomea mradi huo wenye thamani ya milion 160 kwasababu ya kutosemewa mapato na matumizi ya michango yao wanayotoa na kuhisi kuwa naibiwa hivyo wanataka hatua zichukuliwe kwa viongozi wote wanahusika katika kuzila fedha za michango yao.