Ijumaa , 6th Jun , 2014

Watoto wenye ulemavu wa ngozi wamesema kitendo cha wao kuhifadhiwa katika makambi maalum ni cha unyanyasaji na kuchangia kuwaongezea zaidi ulemavu na kuwatenga na watoto wenzao katika jamii.

Watoto wenye wakiwa katika mkutano wa Baraza lao mkoani Mbeya

Watoto wenye ulemavu wa ngozi wamesema kitendo cha wao kuhifadhiwa katika makambi maalum ni cha unyanyasaji na kuchangia kuwaongezea zaidi ulemavu na kuwatenga na watoto wenzao katika jamii.

Watoto hao wamesema hayo katika mkutano wa baraza la watoto wenye ulemavu mkoani Mbeya wa kujadili changamoto zinazowakabili, licha ya kulaani vitendo vya ukatili dhidi yao yakiwemo mauaji lakini wanasema wasitengwe na jamii na kwa wale wanaosoma waishi katika mabweni na watoto wenzao

Afisa ushawishi na utetezi wa programu ya mabaraza ya watoto nchini Tanzania Bwana Josphat Tona amesema tatizo la mauaji na ukatili dhidi ya watoto wenye ulemavu linaweza kukomeshwa na watanzania wenyewe bila kutegemea mataifa. mengine.

Naye afisa usatwi wa jamii mkoani mbeya bi. Aika temu amesema licha ya kuwepo kwa sheria namba 9 ya mwaka 2010 ya watu wenye ulemavu, lakini ukatili dhidi ya kundi hilo ni mkubwa.
Zaidi hawa hapa watoto wenye ulemavu pamoja na Afisa Ustawi wa Jamii.

Juni 16 kila mwaka maadhimisho ya siku ya mtoto yanafanyika barani Afrika na Tanzania ni miongoni mwa nchi waasisi wa mpango wa utekelezaji wa watu wenye ulemavu na mwanachama wa taasisi ya marekebisho kwa watu wenye ulemavu na ilisaini mkataba kuhusu ulinzi na uboreshaji wa haki na heshima kwa watu wenye ulemavu.